
Kuongezwa Kwa Muda Wa Maombi ya Ufadhili 2024/2025
2/11/24, 09:00
Hope Grants Africa inapenda kuwafahamisha Waombaji wa ufadhili na Umma kwa ujumla kuwa muda wa kuwasilisha maombi ya ufadhili kwa ajili ya elimu ya msingi mpaka chuo na ufadhili kwa ajili ya wafanya biashara wadogo umesogezwa mbele hadi tarehe 10 Novemba, 2024.

Hatua hii imechukuliwa ili kuwapa fursa wale ambao kwa sababu mbalimbali hawakuweza kufanya maombi ya ufadhili katika muda uliokuwa umepangwa.
Itakumbukwa kuwa, awali Hope Grants Africa ilianza kupokea maombi ya ufadhili kwa njia ya mtandao tarehe 17 September, 2024 na mwisho wa kuwasilisha maombi ulipangwa kuwa tarehe 01 Novemba, 2024.
Waombaji wa ufadhili kwa mwaka 2024/2025 ambao hawajakamilisha maombi yao wanashauriwa kukamilisha na kuwasilisha maombi yao ya ifadhili ndani ya muda ulioongezwa.
Hope Grants Africa inasisitiza kuwa hakutakuwa na muda mwingine wa nyongeza baada ya tarehe 10 Novemba, 2024. Kwa taarifa zaidi tafadhali tembelea tovuti rasmi ya Hope Grants Africa https://www.hopegrantsafrica.com/apply-now